KOCHA WA AZAM AHAHA KUWABADILI WACHEZAJI WAKLE KISAIKOLOJIA

BAADA ya kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani, kocha wa timu ya Azam, Aristica Cioaba anafanya kazi ya kutuliza akili za wachezaji ambao wanaonekana kukata tamaa msimu huu.

Azam hawana tumaini lolote baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe La FA huku nafasi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa mikononi mwa timu za Simba na Yanga.

Kocha wa timu hiyo alisema kuwa amewambia wachezaji wake kusahau kilichotokea kwenye mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la FA na badala yake wawaze mechi za Ligi Kuu Bara ambazo zimesalia.

“Tuna kikosi kizuri isipokuwa Mao yupo Denmark kwenye majaribio, najaribu kuwasihi wasahau kilichotokea kwenye mchezo wetu wa nusu fainali ya Kombe la FA,” alisema kocha huyo. 

“Nawataka wasahau kabisa mambo yaliyopita kwasababu kila mmoja anajua kilichotokea kwenye mechi yetu dhidi ya Simba ambapo palikuwa na mambo mengi yasiyokuwa ya kimpira,” aliongeza kocha huyo.


Timu ya Azam ililazimika kucheza pungufu uwanjani baada ya kiungo Abubaka Salum "Sure Boy" kulimwa kadi nyekundu.

No comments