KOCHA WA MBEYA CITY ASEMA YANGA ILISTAHILI KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU MSIMU HUU

KOCHA wa timu ya Mbeya City, Kinnah Phiri amesema kuwa klabu ya Yanga ilistahili kupata ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye mechi za mzunguuko wa pili.

Phiri alisema kuwa ni jambo la kushangaza kwa klabu kubwa kama Yanga yenye wachezaji wazoefu kukosa ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu bara.

“Tangu mzunguuko wa pili kuanza dalili zilionekana mapema kwamba Yanga imepania kutetea ubingwa wake, ni timu iliyokuwa ikicheza kitimu na kikosi chake kimejaza wachezaji wazoefu kuliko kikosi chochote hapa nchini,” alisema kocha huyo.

“Unawezaje kukosa ubingwa kama umejaza wachezaji wazoefu kwenye kikosi chako ambao wamekaa pamoja kwa muda mrefu na wanacheza mechi nyingi zaidi ndani na nje ya nchi,” aliongeza kocha huyo.


Kocha huyo amepania kukisuka kikosi chake upya baada ya msimu huu mambo kwenda tofauti na matarajio yake huku timu yake ya Mbeya City ikigeuzwa ngazi ya yanga kuelekea kubeba ubingwa.

No comments