KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA ATABIRI KOMBE LA LIGI KUU KUTUA MSIMBAZI MSIMU HUU

KUNA mtu mmoja katika Simba aliyefanya kazi ya maana sana akaondoka katika mazingira ambayo hayakuwa na maana sana.

Huyu ni Mzungu muingereza Dylan Kerr ambaye alikuwa kocha wa kikosi hicho cha Wekundu wa msimbazi.

Kerr ambaye kwa sasa anafanya kazi yake ya ukocha nchini kwao Uingereza amehojiwa na kusema kwamba pamoja na mizengwe yote lakini anaamini Simba ndio wataibuka mabingwa wapya wa soka hapa nchini.

Kerr amesema kwamba watu wengi wanaipa Yanga nafasi ya kuwa bingwa lakini yeye kama mtaalamu wa ufundi inaiona Simba itakuwa bingwa na wala si Yanga.

“Siku zote timu bora ndio inaku wa bingwa. Naiombea sana iwe bingwa na siku zote nimekuwa nikitamani iwe hivyo sio tu kwasababu naipenda Simba bali kwavile naiona kuwa ni timu bora,” amesema Kerr.

Kocha huyo kwa sasa anaiona timu ya Chesterfield ya nyumbani kwao inayoshiriki League Two ambayo ni ngazi ya nne katika mfumo wa Ligi za England.

Kerr, beki wa kushoto wa zamani wa timu ya Ligi Kuu ya Leeds United ya England amesema kwamba bado anaipenda Simba na anaowaombea waweze kuwa mabingwa wa Ligi msimu huu.

Pamoja na kwamba baadhi ya watu katika Simba hawakupenda kuendelea na Kerr lakini alisaidia sana kusuka stamina upya katika kikosi hicho akisaidiwa na aliyekuwa msaidizi wake Seleman Matola.


“Leo unaweza kufukuzwa mahali fulani lakini ajabu ya soka ni kwamba kesho unaweza kurejeshwa na kufanya kazi ya maana zaidi. Kwangu mimi nikiambiwa kwamba nirejee Simba niko wakati wowote” amesema Kerr.

No comments