KUJIUZURU KWA MANJI YANGA KWAZUA TAFRANI MTAA WA JANGWANI

HATUA ya kujiudhuru kwa mwenyekiti wa Yanga limeibua hisia kali kwa wanachama na wadau wa klabu hiyo wengi wakisema hawakubaliani na uamuzi huo lakini kumbe kilichomng’oa ni hatua ya kuingia mkataba na Sportpesa hivi karibuni ambao umeonekana kuwa na mambo ambayo hayakumpendeza.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba Manji amechukizwa na hatua ya klabu hiyo kuingia mkataba na kampuni ya Sportpesa ambao watendaji wake waliokuwa wakisimamia mkataba huo wameshindwa kusimamia mambo muhimu katika kurekebisha katika kuingia mkataba huo.

Mmoja wa mabosi wa Yanga ameielezea saluti5 kwamba Manji ameusoma mkataba huo na kuona bora klabu hiyo ingekubali hatua ya uwekezaji ambao alitaka kuufanya, ambao ulikuwa ukiipa timu faida kubwa huku hasara ikikosekana tofauti na mkataba wa kampuni hiyo ambao umeonekana na mapungufu mengi.

Mambo ambayo Yanga imeyabaini ni kwamba mkataba huo unamruhusu mdhamini kutumia logo ya klabu hiyo pale anapoona inafaa huku pia akitakiwa kujulishwa haraka hatua yoyote ya kuingia udhamini kati ya klabu na udhamini mwingine mpya yoyote.

Pia mkataba huo umeonyesha kwamba Yanga inatakiwa kuiruhusu klabu kushiriki mashindano maalum yatakayoandaliwa na mdhamini mara mbili kwa mwaka bila kukosa wakati wowote wakiarifiwa kuwepo.


Aidha Yanga inatakiwa kutoa kiasi cha tiketi 380 kwa kila mchezo watakaokuwa wanacheza nyumbani kumpa mdhamini husika ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya zile 50 walizokuwa wakitoa kwa udhamini wa awali TBL ambazo nazo zilionekana nyingi kwa Yanga na kupunguzwa mpaka 25.

No comments