Habari

KUMBE DIDA WA TIMES MDOMO WA BURE TU, SOMA HAPA UPATE KILA KITU

on

MTANGAZI wa kipindi cha “Mitikisiko
ya Pwani” cha Times Fm, Khadija Shaibu “Dida” ameweka wazi kuwa “mdomo” wake
huishia studio anakosikika akitangaza kwa mbwembwe na mikwara, ambapo amesema
kuwa hana ubavu wa kupigana kama wengi wanavyodhani.
Akiongea na saluti5, Dida
amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakimchukulia kama mwanamke mshari anayependa
ugomvi, huku akiwa na nguvu za kuzichapa na yeyote atakayelianzisha kwa wakati
anaotaka.
“Mimi bwana sina nguvu za
kupigana, tena naogopa kabisa ngumi. We ukitaka kujua kuwa mi ni mwoga jaribu
kuchokoza ugomvi mbele yangu uone nitakavyotimua mbio na kukuachia vumbi nyuma,”
amesema Dida.

“Tena usije ukajishaua
kuchokozana na mtu huko halafu eti ukategemea una dada yako Times Fm sijui
anaitwa Dida, lako hilo. Ukinipigia simu nitaitika kama niko usingizini vile na
nitazuga nimelala kabisa,” aliongeza mtangazaji huyo mwenye maneno mengi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *