KWA DONGO HILI ARSENAL LAZIMA WAMCHUKIE ROY KEANE ILA MAN UNITED WATACHEKELEA

Roy Keane amesema kama Jose Mourinho atapanga kikosi dhaifu Jumapili, bado Manchester United itaifunga Arsenal.
Mouriho ameshaweka wazi kuwa amekata tamaa ya United kumaliza katika 'top four' ya Premier League na akasema atapanga kikosi dhaifu katika mchezo dhidi ya Arsenal ili kuweka nguvu  Europa League.
United inakwenda Emirates Jumapili huku pia ikikabiliwa na mchezo wa marudiano wa Europa League Alhamisi ijayo dhidi ya Celta Vigo.
Roy Keane nyota wa zamani wa United ambaye kwasasa ni mchambuzi wa soka, anasema uamuzi wa Mourinho  ni sahihi na bado anaamini timu dhaifu ya Manchester United inaweza ikazoa pointi tatu Emirates.
Keane anasema Arsenal haiko vizuri na inatakiwa kufumuliwa na kufanyiwa mabadiliko makubwa msimu ujao.

No comments