LIPULI FC KUMALIZANA NA SELEMANI MATOLA WIKIENDI HII KWA AJILI YA KUINOA

TIMU ya Lipuli ya Iringa imefanya mazungumzo ya awali na aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola kwa ajili ya kumlambisha mkataba wa kuinoa timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.


“Tuna asilimia 90 hadi 100 kwamba ndie atakayekuja kuwa kocha mkuu ambapo ndani ya siku mbili hizi viongozi watakuwa wameshasaini nae mkataba,” alisema mwenyekiti wa timu hiyo, Abdul Majeki.

No comments