LIPULI FC YASEMA HAITASHUGHULIKA NA USAJILI WA WACHEZAJI WA KIGENI

TIMU ya Lipuli kutoka Iringa imesema itawekeza zaidi katika wachezaji wazawa tofauti na timu nyingi, hususan kubwa kubwa ambazo zina wachezaji wengi wa kigeni wanaolipwa ghali huku utendaji wao dimbani ukiwa sana na wale wa nyumbani.

“Unajua tumejifunza kutoka kwenye timu zetu kubwa kama vile Yanga, Simba na Azam ambao wamekuwa wakisajili zaidi wachezaji wa kigeni, lakini ukiangalia usajili wa wachezaji wa kigeni na uwezo wanaouonyesha uwanjani ni tofauti,” amesema mwenyekiti wa timu hiyo, Abdul Majeki.

“Dhamira yetu sisi hatutaki tushindane tu kwenye Ligi, hatusajili labda kwa sababu tu timu fulani imesajili wakati viwango vinafanana. Ukiangalia hata tu kwenye timu kama Mbao FC imeonyesha ushindani ingawaje haina usajili wa kutisha wa wachezaji wa kigeni.”


“Hata katika benchi la ufundi, ukiangalia hela wanazolipwa makocha wa kigeni na mchezo wanaouonyesha uwanjani unakuta ni vitu viwili tofauti, kwahiyo sisi tutaelekeza nguvu zetu kubwa katika kusajili wachezaji wazawa,” alisema.

No comments