LWANDAMINA AANZA KUIANDAA YANGA KWA AJILI YA MICHUANO YA KIMATAIFA

BAADA ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza ndani ya msimu wake wa kwanza, kocha Geogle Lwandamina ameanza kuitengeneza timu hiyo kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Yanga ilitangazwa kuwa bingwa mara tatu mfululizo baada ya kukaa kileleni dhidi ya simba kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa hivyo kupata uwakilishi kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

“Tunamshukuru Mungu kufikia kwenye nafasi hii tuliyopata baada ya kupambana katika mazingira magumu lakini mwisho wa siku tumekuwa mabingwa,” alisema kocha huyo.

“Tunafahamu ukubwa wa jukumu lililopo mbele yetu kwenye michuano ya kimataifa na sasa tumekaa katika mkao wa kulitazama hilo ili kuweza kufikia hatua kubwa zaidi.”

“Ni michuano migumu kidogo, tunalazimika kufanya usajili na kufanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza kwenye Ligi na hasa eneo la kiungo, beki na ushambuliaji,” aliongeza raia huyo wa Zambia.

No comments