LWANDAMINA AJIPONGEZA KWA KUNUKIA KUCHUKUA UBINGWA YANGA... atamba mambo matamu zaidi yanakuja msimu ujao

KOCHA wa Yanga, Geogre Lwandamina amewaambia mashabiki wa Yanga kwamba hatua yao ya kuchukua taji la ubingwa ni kama kawaonyesha hatua ya mafanikio lakini mambo matamu zaidi yanakuja msimu ujao.

Akizungumza na saluti5 Lwandamina alisema umoja na ushirikiano ndani ya Yanga ndio hatua iliyoleta ubingwa huo licha ya changamoto nyingi walizopitia katika msimu huu.

Lwandamina alisema anataka kusuka kikosi cha nguvu katika kuelekea msimu ujao ambapo tayari ameshafanya kazi kubwa ya kushauri uongozi wa juu wa klabu hiyo katika wachezaji wa maana anaowataka ambao endapo watapatikana msimu ujao utakuwa na mafanikio makubwa na ubingwa utatua mapema tu.

“Tumekuwa na changamoto nyingi za maisha ya hapa lakini umoja wetu na usirikiano wa wanachama na uongozi leo (jana) umetufanya tufurahie mafanikio haya lakini huu ni kama mwanzo na mambo mazuri yatakuja katika msimu ujao tutakaoanza pamoja,” alisema Lwandamina ambaye amepoteza mechi moja tu katika Ligi tangu atue  Yanga.

Katika kufanyia kazi usajili huo, mtandao huu unajua kwamba kocha huyo amefanya kikao kizito wiki hii na vigogo wanaosimamia usajili ambapo katika majina ya wachezaji anaowataka uongozi umewakubali wote na kuanza harakati za kuwanasa.


Katika orodha hiyo Lwandwamina amewaorodhesha mabeki watatu, viungo watatu na washambuliaji wawili ambao bado majina yao yamefanywa siri kubwa kuhofia kuzidiwa kete.

No comments