LWANDAMINA AMKATAA JOHN BOCCO KWENYE MAPENDEKEZO YA USAJILI YANGA

KOCHA wa Yanga, George Lwandamina amewashangaza vigogo wa kamati ya usajili akiwaambia haoni sababu ya kumsajili aliyekuwa nahodha wa Azam FC, John Bocco, lakini akawaambia watamuona mshambuliaji hatari katika ripoti yake ambapo Bocco chamtoto.

Bocco ameachwa na klabu yake ya Azam baada ya mkataba wake kumalizika ambapo haraka jina lake likapelekwa Yanga aweze kupata nafasi, huku pia vigogo wa Azam wakitaka kumpeleka Simba.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba kikao kilichofanyika kati ya kocha huyo na vigogo wa kamati ya usajili, ni kwamba Mzambia huyo amegoma kusajiliwa kwa Bocco akisema si aina ya mshambuliaji anayemtaka.

Bosi huyo amesema tayari anawajua washambuliaji wawili anaowataka katika kichwa chake ambapo mmoja ni mzawa na mwingine ni wa kigeni ambao watakapotua Yanga safu ya ushambuliaji itakuwa mwiba mkali.

Kigogo huyo alisema, Lwandamina ambaye hajaungana na kikosi chake katika ziara yao ya mikoani kupeleka Kombe, ameendelea kumalizia ripoti yake ambayo itatua kwa Kamati hiyo siku yoyote kuanzia wiki hii.

“Tulikutana na kocha Lwandamina tukamuwasilishia jina la Bocco kwamba ni mshambuliaji ambaye yuko huru, lakini katika hali ya kujiamini kabisa, akatuambia si aina ya mshambuliaji anaemtaka,” alisema bosi huyo.


“Ametuambia kwamba anataka kuongezwa washambuliaji wawili na mmoja kati ya hao ni mzawa lakini mwingine ni wa kigeni ambapo atakapomaliza kuandaa ripoti yake tutawaona lakini akaongeza kwamba endapo tutawapata msimu ujao tutakuwa na safu bora yenye makali ya ushambuliaji.”

No comments