LWANDAMINA ASEMA HATMA YA YANGA KUTETEA UBINGWA WA LIGI KUU IKO MIKONONI MWA PRISONS

PAMOJA na uwepo wa wachezaji majeruhi kwenye kikosi cha Yanga, kocha wa timu hiyo, George Lwandamina amesema kuwa hatima ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara itaonekana baada ya mechi ijayo dhidi ya Prisons ya Mbeya.

Yanga ambayo Jumapili ilicheza na Mbao FC ya jijini Mwanza katika hatua ya nusu fainali, inatarajia kucheza na Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao utacheza kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Najua Prisons watakuja kwa namna tofauti baada ya kuwafunga kwenye mchezo wa FA, watacheza kwa kukamia mchezo, tumejipanga kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema kocha huyo mwenye rekodi ya kusisimua Afrika.

“Tunaweza kuona mwanga wa ubingwa baada ya mechi ya Prisons, ni mchezo muhimu zaidi kwetu ambao inatubidi tuhakikishe tunahondoka na pointi zote 3,” aliongeza kocha huyo. 

Yanga inatarajia kucheza na Prisons Mei 6, katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam huku mabingwa hao watetezi wakiwa na kumbukumbu ya ushindi ya mabao 3-0 katika mchezo wa Kombe la FA.        

No comments