LWANDAMINA AWACHEKA SIMBA SC KUISHTAKI TFF FIFA... awaambia "mmebugi men"

KOCHA wa Yanga, George Lwandamina amewacheka Simba katika akili yao ya kulishitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), huko FIFA akisema kwamba wamebugi kwa kuwa wao sio wanaotakiwa kuwasiliana na FIFA.

Akizungumza na saluti5, Lwandamina alisema Simba haiwezi kupata chochote katika safari yao ya kutaka ubingwa kutoka FIFA kwa kuwa wao sio waliotakiwa kuwasiliana na mamlaka hiyo badala yake waliotakiwa kufanya hivyo ni TFF.

Lwandamina ambaye kitaaluma ni mkufunzi wa CAF, alisema mbali na hilo, Simba pia ilitakiwa kuwasilisha malalamiko yake ndani ya Siku 21 tangu maanuzi ya kupokonywa haki yake ifanyike kitu ambacho ni wazi watani wao hao walichelewa kupeleka malalamiko yao.

Alisema, haoni wapi Simba itapata kile wanachotarajia katika safari hiyo ambapo anavyoona FIFA itatulipia mbali malalamiko yao kwa kufanywa nje ya utaratibu.

“Kuna mambo mengi Simba walitakiwa kuyafanya, nimeona zile nyaraka ambazo Simba wamezipeleka FIFA lakini zinaonyesha wamepeleka wao kitu ambacho sio sahihi, Shirikisho la hapa ndio lililotakiwa kuwasiliana na FIFA sio wao,” alisema Lwandamina.


“Ukiacha hilo, nimeona wiki iliyopita ndio Simba wamepeleka malalamiko yao lakini utaratibu unaonyesha Simba walitakiwa kufanya hivyo ndani ya siku 21 tangu maamuzi husika yafanyike.

No comments