MAANDALIZI YA MWISHO YA MSTAHIKI MEYA NGUMI ZA RIDHAA YAKAMILIKA

CHAMA cha ngumi za riadha mkoani Dar es Salaam (DABA), Kimesema maandalizi ya mwisho ya mashindano ya Kombe la mashindano ya mstahiki Meya wa jijini Dar es Salaam, sasa yamekamilika.

Maandalizi hayo ni pamoja na majiji ya ndani na nje ya nchi yaliyopewa mwaliko kwa ajili ya kuthibitisha ushiriki waweze kuthibitisha ambapo mwisho ni leo mei 15.

Katibu mkuu wa DABA, Wamboi Mangore alisema kuwa majiji yenye nia ya kuungana pamoja yaweze kuthibitisha ili kutoa fursa kwa kamati kupanga ratiba mapema.

Alisema, lingine ni pamoja na kuweka nafasi kwa kamati kuandaa mazingira ya kufahamu idadi ya washiriki watakaoshiriki mashindano hayo.

Mangore alisema tayari majiji ya ndani na nje yalipewa mialiko ya ushiriki ili yaweze kutoa uthibitisho.

Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha uthibitisho huo unafanyika kwa muda uliopangwa ili kukisaidia chama kufanya maandalizi ya ratiba na mambo mengine.

“Kwa kuwa muda bado upo na milango ipo wazi, tunatarajia majiji tuliyoyapa mialiko kwa siku zijazo yatathibitisha ili kuwepo na ushindani mkubwa kwa mwaka huu,”alisema Mangole.

Katibu huyo alisema kuwa mbali na kutoa mialiko hiyo kwa majiji ya nje ya mkoa wa Dar es Salaam, wilaya tano zilizopo katika jiji la Dar es salaam zimealikwa kushiriki pamoja na taasisi za majeshi ya ulinzi na usalama.

No comments