Habari

MABEKI WAWILI WA MBAO FC WAWANIWA KIKOSI CHA KOCHA LWANDAMINA YANGA

on

YAANI ni kama vile Yanga inataka kuibomoa timu ya Mbao Fc kwa
kuwachukua mabeki wawili wa kazi akiwemo Jamali Mwambeleko ambaye amekuwa
na msimu mzuri kwa timu yake.
Beki huyo anayemudu kucheza kama beki wa kushoto, amekuwa ni msaada mkubwa kwa Mbao lakini pia anaweza kucheza kama kiungo wa kati.
Yanga inataka kuimarisha nafasi ya beki wake wa kushoto  ambapo endapo itamnasa kinda huyo ni
wazi mkongwe Oscar Joshua hatakuwa sehemu ya timu hiyo kwa msimu  ujao akisalia Haji Mwinyi.
Mbali na mwembeleko pia Yanga inataka kumng’oa Mghana Asante Kwasi anayecheza beki wa kati ambaye amekuwa beki kisiki kwa timu timu hiyo.

“Kweli tunataka kuwachukua hao
wawili, tumeanza kuwafatilia kwa muda
mrefu lakini (Jumamosi) tumejiridhisha kwamba wanatufaa,” alisema bosi mmoja wa
Yanga.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *