MAJIMAJI WACHEKELEA "AFADHALI" YA KUNUSURIKA KUSHUKA DARAJA

KOCHA wa timu ya Majimaji, Kali Ongala amesema kuwa hakuna aliyetaraji kama timu yake itakuwa salama mpaka kufikia wakati huu ambapo hawako kwenye orodha ya timu tatu zinazopigiwa mahesabu ya kushuka daraja.

Majimaji haipo kwenye timu tatu za chini ambapo imesimama juu ya timu tano zinazopigania kutoshuka daraja msimu huu huku ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 32.

“Najua kila mmoja alituweka sehemu mbaya ya kushuka daraja msimu huu lakini mpaka sasa unaweza kuona mambo yanavyobadilika kila kukicha na kila kitu kinakwenda sawa,” alisema kocha huyo.

“Ndio. Ni kweli Ligi imekuwa ngumu na hasa unapotakiwa kupambana na timu zenye bajeti kubwa ya usajili, lakini nashukuru tumepambana mpaka kufikia hapa tulipo. 
Tulikuwa ni timu iliyohesabiwa kushuka tu,” aliongeza.


Balaa la kushuka daraja msimu huu linaonekana kuziandama timu za JKT Ruvu, Toto Africa na Ndanda ambazo zinakamata nafasi tatu za mwisho.

No comments