Habari

MANCHESTER CITY HAO KIULANI TOP FOUR YA LIGI KUU YA ENGLAND

on

Manchester City ni kama imejihakikishia kumaliza katika nafasi nne za
juu za Premier League baada ya kuinyuka West Brom 3-1.
City sasa ipo njiani kumaliza katika nafasi ya tatu au ya nne
kutegemea na matokeo watakayoyavuna kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Watford ambayo haina cha kupoteza katika mechi hiyo.
Kama itashinda mchezo wa mwisho, basi City itamaliza katika nafasi ya
tatu, ikitoa sare itakaa nafasi ya tatu au nne kutegemea na matokeo ya
Liverpool, lakini ikifungwa basi asubiri matekeo ya Arsenal itakayotakiwa kushinda kwa magoli dhidi ya Everton na Liverpool dhidi ya Middlesbrough.
Wafungaji wa City walikuwa ni Jesus 27, De Bruyne 29 na Toure 57  wakati lile la West Brom likipitia kwa Robson-Kanu.
Manchester City
(4-1-4-1):
Caballero, Fernandinho, Kompany (Stones 77), Otamendi, Kolarov, Toure
(Fernando 81), Gabriel Jesus, De Bruyne, Silva (Zabaleta 62), Sane, Aguero
West Brom
(4-1-4-1):
Foster, Dawson, M Wilson (McClean 52), Evans, Nyom, Yacob, Chadli,
Fletcher, Livermore (Morrison 65), Brunt, Rondon (Robson-Kanu 71)

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *