MANCHESTER CITY YAIFUNGA ‘KINGEKEWA’ LEICESTER CITY NA KUNUSA ‘TOP FOUR’


Manchester City imeifunga Leicester City 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England na kuzidi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumaliza kwenye ‘top four’.

Mabao ya Manchester City yalifungwa na David Silva katika dakika ya 29 na Jesus aliyefunga dakika ya 36 kwa mkwaju wa penalti wakati goli pekee la Leicester lilikwamishwa wavuni na Shinji Okazaki kunako dakika ya 42.

Hata hivyo Leicester walipoteza nafasi ya dhahabu baada ya Riyad Mahrez kufunga bao la penalti dakika ya 77 lakini mwamuzi Robert Madley akalitaa.

Wakati Mahrez anapiga mpira huo wa adhabu aliteleza na bila kutarajia akajikuta ameugusa mpira mara mbili kabla ya kuujaza wavuni na hivyo mwamuzi akaamuru iwe ‘free kick’ kuelekea Leicester City.

MANCHESTER CITY (4-3-3): Caballero 6; Fernandinho 6, Kompany 7, Otamendi 7, Clichy 5.5; Toure 6.5, Silva 7.5, De Bruyne 6.5 (Zabaleta 82); Sterling 6.5 (Aguero 78, 6), Jesus 6 (Navas 90), Sane 6.5.

LEICESTER CITY (4-4-1-1): Schmeichel 6.5; Simpson 6, Benalouane 5.5, Fuchs 6, Chilwell 5.5; Mahrez 7, King 6 (Amartey 68, 6), Ndidi 7, Albrighton 6.5 (Gray 80); Okazaki 7 (Slimani 73, 6); Vardy 6.5.

No comments