MANCHESTER UNITED YAAGA RASMI TOP FOUR …yapigwa 2-1 na Tottenham


Manchester United imeaga rasmi mbio za kutaka kumaliza kwenye top four ya Premier League baada ya kufungwa 2-1 na Tottehnam.

Tottenham ambayo ilikuwa ikicheza mchezo wake wa mwisho kwenye uwanja wa nyumbani White Hart Lane ambao hawatautumia tena msimu ujao, walitibua mbinu za United kwa kufunga bao la mapema katika kila kipindi.

Victor Wanyama alifunga bao la kwanza dakika ya 6 huku Harry Kane akitupia la pili dakika ya 48, kabla ya Wayne Rooney hajaifungia United bao la kufutia machozi dakika ya 71.

United  imebaki nafasi ya sita ikiwa na pointi 65 ambazo hazitoshi kuifikia Liverpool wala Manchester City  kama itashinda michezo yake miwili ya mwisho.

Hiyo inamaanisha kuwa United itamaliza ligi katika nafasi ya sita au ya tano kwa vile Everton inayoshika nafasi ya saba na pointi 61 hataiweza kubadili msimamo wa ligi.


Msimu uliopita United chini ya kocha Van Gaal, ilimaliza katika nafasi ya tano kwa kukusanya jumla ya pointi 66.

No comments