MANJI AWATIA TUMBO JOTO WACHEZAJI WANAOMALIZA MIKATABA YAO YANGA

HATUA ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji umewatisha mastaa wengi wanaomaliza mikataba yao ndani ya Yanga na huku wale waliotaka kutua nao wakipotea hewani.

Taarifa kutoka ndani ya Kamati inayosimamia usajili ni kwamba jumla ya kiasi cha sh mil 700 zinahitajika katika kuendesha jukumu la usajili katika kuwaongezea mikataba baadhi ya mastaa wakiwemo Haruna Niyonzima na Thabani Kamusoko.

Bosi mmoja wa Yanga amesema mbali na hilo, pia Kamati yao iliwaweka tayari mastaa wengi kusajiliwa katika kipindi hiki lakini zoezi hilo limekwama kutokana na taarifa za bosi huyo kujiengua.

Endapo wanachama wa Yanga watashindwa kupambana na kuhakikisha bosi huyo anarudi kundini, Yanga inaweza kupata shida kubwa kwa kuzidiwa kete katika usajili ambapo mkataba mpya na Sportpesa ambao klabu hiyo imeingia hauna kipengele ambacho watasaidia katika usajili.

“Kiukweli hili ni pigo kubwa kwetu kama Kamati ya usajili, hatuna tena nguvu za kusema tufanye mazungumzo ya kuwaongezea mikataba wachezaji tunaowahitajika benchi la ufundi katika kuwabakisha,” alisema bosi huyo.


“Pia kuna wachezaji wapya nao usajili wao utazuilika, hakuna atakayekubali kuja hapa bila Manji ambaye angekuwa na uhakika na malipo yao, nafikiri wana Yanga wanatakiwa kupambana kuhakikisha jamaa anabaki.”

No comments