MARTIN SOSPETER AREJESHEWA UMENEJA TWANGA PEPETA …Zonte naye arejeshwa


Mameneja wawili waliowahi kufanya vizuri ndani ya ASET inayomiliki Twanga Pepeta, Martin Sospeter na Zonte Mahundu wamerejeshwa kundini ili kuongeza ufanisi wa bendi hiyo.

Martin (picha kubwa) aliyeitumikia Tam Tam na baadae Twanga Pepeta, anarejea Aset baada ya kufanya kazi na Mashujaa Band kwa miaka kadhaa.

Naye Zonte (picha ndogo) aliyekuwa meneja wa Tam Tam kabla kuachana na mambo ya muziki, alijenga jina zaidi kupitia FM Musica International na baadae FM Academia.

Taarifa ya wazi ya meneja wa Twanga Pepeta Hassan Rehani imesema hivi: Kuanzia leo Meneja Martin na Meneja Zonte wanarudi rasmi kuongeza nguvu ndani ya menejiment ya Aset.

Naomba tuwape ushirikiano waa kutosha watakapokuwa wakitimiza majukumu yao.

No comments