MASHABIKI WA SIMBA WAJIPANGA KUHAKIKISHA WANAIRARUA MBAO FC

BAADHI ya mashabiki wa Simba nao sasa wamemeibuka na kusema kwamba wanataka kuhakikisha kwamba timu yao inaibuka na ushindi katika mechi yao dhidi ya Mbao FC na nguvu ya kuisaidia timu ni kubwa zaidi.

“Tunataka kuhakikisha kwamba Simba inakuwa bingwa kwa kishindo, tunapata ushindi na kutwaa ubingwa wa FA,” amesema mmoja wa wanachama wa Simba, Ally Mahamoud.

Lakini pia mwanachama huyo amesema kwamba kwa umoja wao kama wanachama, wameunda kikosi kazi ambacho kimeanza mchakato wa kuongeza nguvu katika kikosi cha Simba ili kuhakikisha kwamba wanawapa hamasa kubwa wachezaji kuibuka na ubingwa.

“Tunajua kwamba tunacheza na Mbao FC, lakini pia tunacheza na akili za watu wengine, lazima tujikusanye na kuweka utaratibu ambao hakuna anayeweza kuihujumu Simba,” amesema mwanachama huyo.


Amesema kwamba matawi yote ya Simba yameanza mchakato wa kuhakikisha timu yao inapata ubingwa lakini pia inatwaa uchampioni wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

No comments