MASHABIKI WA SOKA WAMKOSOA MALINZI KOPOSTI PONGEZI ZA RAIS WA FIFA KWA UBINGWA WA YANGA

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi juzi aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwmba rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino ameipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.

Hata hivyo, wapenzi na mashabiki mbalimbali wa mpira wa miguu wamemshambulia wakisema anashindwa kuficha hisia zake kwa mapenzi yake kwa Yanga.

Katika baadhi ya Twitter za mashabiki hao, wengi wao wamemlaumu na kumshutumu Malinzi kuwa rais wa FIFA huwa hana muda wa kupongeza klabu zinapotwaa ubingwa.

Mashabiki hao wamesema kwamba Malinzi amedanganya kwa sababu anajua kwamba Simba wana rufaa yao huko FIFA wakilalamikia pointi zao walizoporwa na TFF.

Mashabiki hao wameonekana kukerwa na ujumbe huo wa Malinzi wakisema kwamba bora rais huyo wa TFF achague kuwa kiongozi wa Yanga.

Hata hivyo, Malinzi amemjibu mmoja wa mashabiki hao aliyetaka rais huyo aonyeshe barua hiyo ya rais wa FIFA akisema kwamba barua hiyo itatumwa kwa Yanga ambao ndio wataamua kuiweka hadharani au la.    

No comments