'MASHARTI' ALEXIS SANCHEZ ARSENAL UTATA MTUPU


Alexis Sanchez anataka kucheza Champions League msimu ujao, hatua inayozidi kuiweka pabaya Arsenal ambayo iko mashakani kupata nafasi ya nne kwenye Premier League.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile bado hajasaini mkataba mpya Arsenal, mazungumzo yakitarajia kuanza tena baada ya fainali ya FA, Mei 27.

Mbali na kipaumbele cha Champions League,  pesa itakuwa kipaumbele kingine ambapo inadaiwa Sanchez anataka mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki, kitu ambacho kwa Arsenal ni mtihani mzito.

No comments