MASHAUZI CLASSIC KUREJEA MANGO GARDEN KWA KISHINDO ALHAMISI HII


Baada ya kushindwa kutumbuiza kwenye ukumbi wao wa nyumbani (Mango Garden) kwa wiki tatu mfululizo, kundi la Mashauzi Classic linarejea kwa kishindo Alhamisi hii.

Mashauzi ilishindwa kufanya onyesho Mango kutokana na mvua zilizokuwa zikiendelea kwa mwezi mzima, lakini sasa ikiaminika kuwa mvua zimeisha, Mashauzi Classic wanasema wanakuja na Usiku wa Zote Kali.

Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa wamebakiwa na Alhamisi mbili kabla ya mapumziko ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na hivyo show zote mbili zilizosalia Mango Garden zitakuwa za kipekee.

“Alhamisi hii Mei 18 tutakuwa na usiku wa zote kali, ambapo zitapigwa ‘hits’ tupu za Mashauzi Classic na Alhamisi ya Mei 25 tutakuwa na onyesho kubwa la Vunja Jungu,” alisema Isha.

No comments