MAVUGO ASIKITIKA KUTOTIMIZA MALENGO YAKE MSIMBAZI MSIMU HUU... awatuliza mashabiki akisema mambo yote msimu ujao

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba raia wa Burundi, laudit Mavugo amesema kwamba malengo yake katika Simba msimu huu uliomalizika hayakutimia.

Mrundi huyo amesema kwamba alipanga kufanya mambo makubwa ndani ya timu hiyo kwa msimu wake wa kwanza lakini changamoto alizokutana nazo zilifanya ashindwe kufikia malengo yake hayo.

Mavugo aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Vital’O ya Burundi, amemaliza msimu wa Ligi Kuu akiwa amefunga mabao saba.

Hata hivyo, straika huyo amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumaliza msimu huu vizuri na bila majeruhi yoyote licha ya mipango yake kwa wana Simba kwenda vibaya lakini anaamini msimu ujao watafanya vizuri zaidi ya hapa.

“Tumeshindwa kuchukua ubingwa lakini bado tuna nafasi kwenye Kombe la Shirikisho, ila kikubwa ni kujituma na kupambana ili malengo yetu yatimie,” amesema Mavugo.


Mavugo aliyepokelewa kwa shangwe kubwa na mashabiki wa Simba kipindi anatua jijini Dar es Salaam, amewaambia wapenzi kuwa wasihofu, anajua msimu ujao watakuwa vizuri sana na watafanya kile ambacho wanakihitaji.

No comments