MAVUGO AWATAKA WACHEZAJI WENZAKE SIMBA SC KUZILINGATIA BENCHI LA UFUNDI

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Laudit Mavugo amewataka wachezaji wenzake kuzingatia mafunzo ya benchi la ufundi.

mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Burundi amesema wachezaji wanatakiwa kuzingatia mafunzo ya makocha ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Akizungumza na mtandao mmoja wa michezo, Mavugo amesema: “Naamini kuwasikiliza makocha ni jambo la msingi kwa sababu wakati tunaanza msimu huu tulikuwa na malengo ya kutwaa ubingwa.”

“Kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu bado tuna nafasi ya kufanya maajabu licha ya kukabiliwa na upinzani kutoka kwa Yanga.”

Mavugo amesema ameimarika vyema tofauti na mwanzo kutokana na ushauri wa makocha wake na wadau wa klabu hiyo kongwe nchini.

“Nataka kumaliza vizuri kwa kujiwekea rekodi nzuri Simba ili hata siku nikiondoka mashabiki wanikumbuke,” amesema.

Mavugo amekuwa mshambuliaji wa kutumainiwa katika Simba akishirikiana na baadhi ya nyota katika kikosi hicho.

No comments