MAYANJA WA SIMBA ASEMA TAMBO ZA YANGA SC MWISHO MWAKA HUU

KOCHA msaidizi wa Simba, Mganda Jackson Mayanja “Miamia” amesema kwamba tambo wanazosema Yanga kila mwaka, zinakaribia kufikia tamati.

Mayanja, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda “The Cranes” amesema kwamba Simba imeweka malengo mazito katika msimu ujao wa Ligi na yanga watakuwa wamenywea.

Amesema kwamba chochote kitakachotokea msimu huu wanakubaliana nacho lakini wameandaa majeshi katika mapambano yajayo kwenye msimu ujao wa Ligi.

“Ukiangalia msimu huu tulianza vizuri lakini mwishoni tukapoteza mwelekeo kidogo na Yanga wakatupita.”

“Kama msimu uliopita tulimaliza nafasi ya tatu, msimu huu tunamaliza wa pili, basi naamini msimu ujao tutakuwa sisi wa kwanza na kuwa mabingwa, hilo linawezekana kabisa kama tukiongeza juhudi tulizozionyesha msimu huu,” amesema Mayanja.


Mayanja amesema kwamba Yanga tambo zao zinaisha msimu huu msimu ujao wasahau ishu ya ubingwa kwani Simba imedhamiria kubeba kila Kombe ambalo litakuwa mbele yao.

No comments