MBAO FC YASISITIZA KUIKAMIA SIMBA SC... yaitahadharisha Simba isitarajie mchekea wa mabao

KIKOSI cha timu ya Mbao FC ya jijini mwanza kimeapa kufa na Simba katika mchezo wa wa fainali ya Kombe la FA ambao utachezwa katika uwanja wa Jamuhuri Dodoma April 27 siku ya Jumamosi.

Simba ambao wamelitolea macho Kombe hilo ili kupata tiketi ya kushiriki kwenye michuano ya kimataifa baada ya kupoteza ubingwa wa Ligi Kuu Bara dakika za lala salama, watakumbana na upinzani mkali kwa timu isiyofungika kirahisi inapokumbana na timu kubwa.

Simba ambayo imekosa kushiriki kwenye michuano ya kimataifa kwa miaka minne sasa, itaingia uwanjani ikiwa na hofu na safu yake ya ulinzi ambayo imekuwa ikiruhusu mabao kirahisi tangu beki wake wa kimataifa David Mwanjare raia wa Zambabwe apate jeraha la goti.

Kocha wa Mbao FC, Ettiene Ndairagije alisema kuwa kikosi chake kitaingia uwanjani kikiwa na kusudio moja tu la kushinda mchezo huo ili kupata nafasi ya Kombe la Shirikisho.

“Hatutaingia uwanjani na hofu, huu ni mchezo wa mwisho ambao utaamua ubingwa. Simba wasitarajie kukutana na urahisi kwenye mchezo huu,” alisema kocha huyo.


Mbao imepanda daraja mwaka jana na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali kwenye michuano ya Kombe la FA dhidi ya Simba ambayo ilipenya baada ya kuifunga Azam kwa bao 1-0.

No comments