MBAO FC YATISHIA KUWEKA HISTORIA YA KUPANDA DARAJA NA KUSHIRIKI MICHUANO YA KIMATAIFA MOJA KWA MOJA

KWA mara ya kwanza kwenye historia ya soka la Tanzania, Mbao FC ya mkoani Mwanza imefuzu kucheza fainali ya FA kwa kuwatoa mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Yanga SC ya jijini Dar es Salaam.

Wakiwa wamepanda daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza, wameweza kufuzu kucheza fainali ya kwanza katika historia yao kwa kuifunga Yanga goli 1-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Goli pekee lililoipa ushindi Mbao lilitokana na kujifunga kwa beki wa kati wa Yanga, Vincent Andrew dakika ya 27 kipindi cha kwanza wakati akiwa katika harakati za kuokoa krosi iliyopigwa na Pius Buswita wa Mbao FC.

Matokeo hayo yameivua Yanga ubingwa wa FA ambao waliutwaa mwaka uliopita kwa kuifunga Azam kwenye mchezo wa fainali.

Mbao watakutana na Simba kwenye mchezo wa fainali, mechi ambayo Simba ndio watakuwa wenyeji kwasababu ndio walikuwa wa kwanza kufuzu kucheza fainali baada ya kuifunga Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.No comments