MENEJA WA ZAMANI WA YOUNG DEE AVIMWAGIA LAWAMA VYOMBO VYA HABARI

MAXIMILIAN Rioba ambaye alikuwa msimamizi wa rapa wa mwanamuziki Young Dee, ametumia akaunti yake ya Twitter kuandika ya moyoni baada ya Young Dee kudai hakuchoka kufanya kazi nae bali yeye ndie alishindwa kuendelea nae.

Max aliandika kupitia akaunti yake kwamba kulikuwa na haja ya vyombo vya habari kutaka kujua pia kwa upande wake ili watu waelewe, kwa kuwa taarifa aliyoitoa young Dee dhidi yao haikuwa sahihi kwani hata yeye aliwahi kutukanwa hadharani.

“Kuna haja ya media kujaribu kubalance taarifa ili wasikilizaji waelewe mambo kama yalivyo na sio kama yalivyosemwa, niliwahi kutukanwa sana, nidhamu ni nguzo ya mafanikio kila mahali, ikivurugwa hiyo hata ungeishi mbinguni ungeporomoka tu,” aliandika Maximilian.


Kumekuwa na hali ya sintofahamu baada ya kutengana kwa rapa Young Dee na Mavimilian Rioba ambao walikuwa wakifanya kazi chini ya kampuni moja.

No comments