MERCY AIGBE AANIKA "MADUDU" YALIYOMFANYA AACHANE NA MUMEWE

STAA wa filamu nchini Nigeria, Mercy Aigbe ameanika kisa kilichosababisha atengane na mume wake, huku pia akianika jinsi ambavyo anapanga kumuweka ndani baada ya kumnyanyasa kwa kipindi kirefu kwa kipigo.

Mercy alikuwa kwenye uhusiano mzito na Lanre Gentry kabla ya kutengana baada ya kuwa na vitimbi vya mara kwa mara.

“Nawezaje kumthamini mwanaume ambaye anajinadi kunipenda lakini tukirudi ndani ananipiga hadi kunivunja mfupa,” alisema staa huyo.

Ndoa ya Mercy na Lanre imeingia doa tangu mwanaume alipotimwe kumshushia mkewe kwa vipigo vya mara kwa mara ndani ya nyumba. 

No comments