MERCY AIGBE AFANYIWA UPASUAJI WA TAYA UINGEREZA

MERCY Aigbe ambaye ni mwigizaji wa filamu nchini Nigeria, ametuma picha zake kwenye mitandao ya kijamii akiwa anafanyiwa upasuaji wa taya nchini Uingereza.

Staa huyo alipata jeraha la taya baada ya kusukumwa kwenye ukuta na mume wake, Baba Olowo walipokuwa wakilumbana.

Ndoa ya wawili hao inaelekea kuvunjwa baada ya kesi hiyo kuwa mahakamani huku Marcy akionekana kutotaka kurejea kwenye ndoa hiyo.

Hata hivyo, safari yake ya Uingereza itaambatana na mapumziko itaambatana na mapumziko ya muda mfupi baada ya mzozo wa ndoa yake.

No comments