MERCY AIGBE AWATAKA WANAWAKE WANAOTELEKEZWA BAADA YA KUZALISHWA WATOTO KUGANGAMALA

STAA wa filamu za maigizo Nchini Nigeria Mercy Aigbe amewataka wanawake wa taifa hilo kutokata tamaa baada ya kufiwa au kutelekezwa na mwanaume waliowazalisha watoto.

Mercy alidai kuwa hata yeye alilazimika kuuza vitu vyake vya thamani ili kulea mtoto aliyempata akiwa na umri wa miaka 22.

“Hakuna haja ya kukata tamaa katika maisha eti kwa kuwa umeachiwa mtoto na mwanaume na hujui la kufanya,” alisema staa huyo.

“Nilipata mtoto nikiwa na umri wa miaka 22 lakini sikukata tama, nilibeba jukumu zima peke yangu bila msaada na kuna wakati nililazimika kuuza vitu vangu vya thamani kwasababu ya malezi.”


Nyota huyo aliowataka wazazi wa Nigeria kuishi maisha ya kutegemea Mungu na sio wanadamu.

No comments