MJUSI SHEMBOZA WA SIKINDE ATAKA RAIS MAGUFULI ASHINIKIZE RADIO NA TV ZIPIGE DANSI KWA 80%, JE YUKO SAHIHI AU KACHEMKA?


Mwanamuziki mahiri wa Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae” Mjusi Shemboza (pichani juu), ametaka Rais John Magufuli awashinikize wakurugenzi wa vituo vya radio na TV vipige muziki wa dansi kwa asilimia 80.

Kama ikitokea wazo la Mjusi Shemboza likapita, maanake ni kwamba asilimia 20 zilizobakia ndio zitabakia kwa muziki wa bongo fleva, muziki wa asili, singeli, muziki wa nje ya nchi na miziki mingine.

Mjusi Shemboza ambaye ni mahiri wa kucharaza gitaa la kati, bass na solo, alitoa wazo hilo kupitia SAKATA RUMBA ambalo ni kundi maarufu la wachambuzi wa muziki wa rumba katika mtandano wa Facebook.

Mwanamuziki huyo alikuwa akichangia hoja ya Msondo Ngoma kurejeshwa serikalini ambayo sasa itamilikiwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania – TUCTA.

Mjusi akaandika hivi: Kiinua mgongo sio ISHU............ISHU ni Mheshimiwa JPJM awalazimishe akina RUGE, MAJIZO na Wakurugenzi wooote wa Redio na Tv kurudisha Airtime 80% ya Muziki wetu huu wa Dansi na Muziki mwingine ili Heshima yetu irudi kama zamani!!
Tuna NYIMBO MPYA
Hatutaki na tumeshachoka kusikia............."Hizi nazo wala Zilipendwa" na Majina ya kutukatisha tamaa
Rudisheni TOP 10.Hata hivyo Saluti5 ilipompigia simu Mjusi Shemboza ili kupata ufafanuzi zaidi, mwanamuziki huyo akasema asilimia 80 alizotaja ni kwaajili ya muziki wa dansi na taarab, halafu 20 ndio ziende kwa aina nyingine ya muziki.

"Haya ni maoni yangu binafsi, sina ubaguzi na muziki mwingine, lakini naona dansi na taarab zinastahili kupata 'airtime' kubwa zaidi.

Je Mjusi Shemboza yuko sahihi au kachemka?


 yuko sahihi kwa maoni yake haya????


No comments