MKUU WA MKOA MWANZA AFANYA TAFRIJA YA KUIPONGEZA MBAO FC

TIMU ya Mbao FC baada ya kufanya maajabu kwenye msimu huu wa Ligi na kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la FA dhidi ya Simba, mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela jana aliandaa tafrija ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo.

Mbali ya wachezaji, tafrija hiyo iliyofanyika majira ya mchana hapo jana, ililihusisha pia benchi la ufundi, viongozi wa timu hiyo, viongozi wa chama na serikali wa mkoa wa Mwanza pamoja na wale wa chama cha mpira wa miguu mkoani humo (MZFA), chini ya mwenyekiti Vedastus Lufano.

Katika hafla hiyo, mwenyekiti wa Mbao, Sori Zefania alitoa neno kuhusiana na timu za Mwanza ambapo alisema kuwa anaomba viongozi, wachezaji na wadau wa soka mkoani humo kushirikiana kuhakikisha mchezo wa timu zao kushaka daraja haujirudii tena.


“Lazima tuwe na mshikamano wa karibu kuhakikisha kuwa Mwanza tunairudisha katika heshima yake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilivyokuwa ikitikisa ikiwa na timu kama Pamba na nyinginezo,” alisema mwenekiti huyo.

No comments