MO IBRAHIM WA SIMBA AFICHUA SIRI YA USHINDI WAO DHIDI YA AZAM FCKIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mohammed Ibrahim “Mo” amesema kuwa wamepata ushindi dhidi ya Azam FC kutokana na jinsi walivyojituma na kusikiliza maelekezo ya kocha wao walipokuwa mapumziko.

Mo licha ya kufunga bao pekee na la ushindi kwa upande wa Simba, alipewa kadi nyekundu na mwamuzi Mathew Akrama kutoka Mwanza baada ya kuonyeshwa kadi ya njano ya pili kwa kumchezea vibaya Shomari Kapombe.

Mo amesema kujituma na umoja katika timu ndio silaha ya ushindi wao licha ya hali ya hewa kuwazuia kucheza kabumbu zuri.

“Tumefurahi kuingia fainali, si unajua kila mtu anataka matokeo mazuri kwenye michuano hii ili kuwakilisha timu katika mashindano ya kimataifa, kama wataingia Mbao basi wajipange sana,” amesema Mo.

Nyota huyo amesema kwamba kukosekana kwake kwenye mechi ya fainali hakutoathiri kitu kutokana na mwalimu kuwa na wachezaji wengine ambao atawapa nafasi.

“Siwezi kuzungumzia sana suala la kadi nyekundu niliyopewa na mwamuzi, nawaachia uongozi wangu wa Simba watalishughulikia.”


Mo ambaye katika mchezo dhidi ya Azam alionekana kubadilisha mtindo wa nywele kwa kunyoa staili ya kijogoo, amesema ni yeye mwenyewe kaibuni kimtaani lakini hajaona mtu akiwa na staili hiyo.

No comments