MO KUMLETA MFADHILI MWINGINE ATAKAYEMWAGA MABILIONI YA PESA MSIMBAZI

MFADHILI na mwanachama wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji “MO” anatarajiwa kumleta katika klabu hiyo mdhamini mwingine ambaye udhamini wake utakuwa wa zaidi ya sh bil 2 kwa mwaka.

Hii  ni wiki moja tu tangu Simba iingie mkataba wa udhamini na kampuni ya Sportpesa ambayo udhamini wake katika Simba ni wa kufikia Sh bil 4.9 kwa miaka mitano.

Taarifa zinasema kwamba Dewji baada ya kumaliza tofauti zake na wenzake sasa ameamua kufanya kufuru ambapo analeta mdhamini ambaye atawekeza katika Simba kiasi cha zaidi ya sh bil 10 kwa miaka mitano.

“Mkataba wa Sportpesa unabaki palepale lakini sasa anakuja mdhamini mwingine ambaye ataweka zaidi ya sh bil 10 katika muda huohuo wa miaka mitano. Hii ni neema kubwa Msimbazi,” kimesema chanzo hicho.

Kama vile haitoshi imedaiwa kuwa Dewji ameitaka Simba wapeleke kwake haraka majina ya wachezaji wote wa kimataifa ili kazi ya usajili ianze.

Ingawa majina ya wachezaji wanaotakiwa yamefanywa siri hadi sasa lakini saluti5 inajua kwamba tayari kuna majina ya Emanuel Okwi wa SC Villa ya Uganda na Kipre Tcheche anayecheza soka Oman.

Simba wanamsajili tena Okwi kwa mara nyingine wakati Kipre aliyekuwa nchezaji wa Azam FC anarejea tena nchini safari hii katika kikosi cha Simba.


“Simba sasa itakuwa timu ya pekee katika Afrika, Dewji ameamua kuibadili kabisa timu na utaona kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu,”amesema mmoja wa watu watu karibu na uongozi wa Simba.

No comments