MO ATIBUA KILA KITU SIMBA... agomea udhamini wa benki na Simba kupoteza pesa nyingi

KIMENUKA Simba SC! Taarifa rasmi kwa sasa ni kwamba baada ya klabu hiyo kuingia mkataba na kampuni ya Sportpesa, mfadhili wao Mohamed Dewji  amewataka kurudisha kiasi cha sh bil 1.5 alizoikopesha timu hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya Simba ni kwamba MO amefikia uamuzi huo akichukuzwa na uamuzi wa rais Evans Aveva ambao walitakiwa kumjulisha bilionea huyo hatua za kuingia mkataba na kampuni hiyo.

Bosi mmoja wa Simba alisema MO aliwakopesha Simba kiasi hicho katika kulipa mishahara ya timu hiyo na mambo mengine ya kuwania ubingwa ikiwa ni makubaliano yao kabla ya kuingia katika hatua ya uekezaji ambao umekwama.

Katika makubaliano ya awali, Simba walimuhakikishia MO kwamba fedha zitafidiwa katika mkataba wa uwekezaji ambao tayari umeshakwama kutekelezwa kwa sasa.

Hatua hiyo ya MO ni wazi italeta vurugu kubwa ndani ya uongozi wa Simba ambapo sasa klabu hiyo italazimika kuingia katika madeni katika juhudi za kulipa fedha hizo.

Inaelezwa pia Simba ilikuwa iingie mkataba na moja ya benki kubwa hapa nchini lakini hatua hiyo ya MO kutakiwa kushirikishwa katika udhamini wowote aligomea udhamini huo na Simba kupoteza fedha nyingi.

No comments