MONACO YAFIKA MWISHO WA RELI, YAUSHINDWA MUZIKI WA JUVENTUS …Higuain moto chini


Monaco ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani, imeambulia kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Juventus katika mchezo wa nusu fainali ya Champions League.

Klabu hiyo ya Ufaransa sasa italazimika kushinda 3-0 ugenini katika mchezo wa marudioano ili kutinga fainali.

Gonzalo Higuain ndiye aliyekuwa mwiba kwa kupachika mabao yote mawili katika dakika ya 29 na 59.

Monaco: Subasic, Fabinho, Glik, Jemerson, Sidibe, Dirar, Bernardo Silva (Toure 81), Bakayoko (Joao Moutinho 67), Lemar (Germain 67), Falcao, Mbappe-Lottin

Juventus: Buffon, Barzagli, Bonucci, Chiellini, Dani Alves, Marchisio (Rincon 81), Pjanic (Lemina 89), Alex Sandro, Higuain (Cuadrado 77), Dybala, Mandzukic.

No comments