Manchester United imeweka mezani mzigo wa pauni milioni 72 ili kupata saini ya kinda Kylian Mbappe lakini kwa mujibu wa ripoti kutoka Italia, ofa hiyo imepigwa chini na Monaco.
Mshambuliaji huyo wa Monaco mwenye umri wa miaka 18, amekuwa gumzo baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu msimu huu.
Sky Sports Italia  imeripoti kuwa Jose Mourinho amejaribu kuwapiku wapinzani wake kwa kupeleka ofa ambayo ingemfanya Mbappe kuwa kinda ghali duniani.
Lakini ripoti zinasema ofa hiyo imekataliwa na vinara hao wa Ligi Kuu ya Ufaransa.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

Oldest posts

 
Top
Nicolaus Trac