"MOYO KAMA MACHO" YA KIVURANDE WA KIBAO KATA YAACHIWA RASMI, YAKUBALIKA KWA KASI

KILE kibao kilichotokea kuzua gumzo kubwa kabla hakijatoka, cha mfalme wa Kibao Kata aliyeamua kuja kwa staili ya mduara, kinachokwenda kwa jina la ‘Moyo Kama Macho’, kimemwagika rasmi wiki iliyopita na kuonekana kukubalika vilivyo.

Kibao hicho ambacho kimesheheni mashairi makali pamoja na mirindimo inayochezeka zaidi, kimeachiwa mwanzoni mwa wiki iliyopita ambapo sasa kinaonekana kukamata vibaya kwenye vituo mbalimbali vya radio na mitandao ya kijamii.

Kivurande mwenyewe alipozungumza na saluti5 amesema kuwa anashukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata kutoka kwa mashabiki tangu siku ya kwanza alipoachiwa kibao hicho.

“Vilevile natoa shukrani zangu za dhati kwa media mbalimbali kutokana na sapoti yao ya nguvu kwangu na naomba waendelee kunipiga tafu hata pale nitakapotoa wimbo mwingine,” amesema Kivurande.

No comments