MOURINHO AIKATIA TAMAA 'TOP FOUR' AWEKA NGUVU ZOTE EUROPA LEAGUE ...kuchezesha 'rizevu' mechi ya Arsenal


Jose Mourinho amefuta matumaini ya  Manchester United kumaliza katika nafasi nne za juu Ligi Kuu ya England na sasa anakiri huenda akachezesha kikosi dhaifu dhidi ya Arsenal Jumapili ndani ya dimba la Emirates. 

Mourinho amezipa kipaumbele mechi za nusu fainali ya Europa League dhidi ya  Celta Vigo akiamini hiyo ndiyo njia pekee iliyopakia ya kumpa tiketi ya kucheza Champions League msimu ujao.

Sare mbili za mfululizo kutoka kwa Manchester City na Swansea katika Premier League, zimepeperusha matumaini ya Mourinho kumaliza 'top four'.

Ingawa United iko pointi moja nyuma ya Manchester City inayoshika nafasi ya nne, lakini inakabiliwa na kibarua kigumu katika mechi zake mbili za ugenini dhidi ya Arsenal na Tottenham.


No comments