Habari

MOURINHO APIGA KIJEMBE CHA MWAKA KWA WACHEZAJI WAKE

on

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameendelea ‘kuugua’ juu ya janga la majeruhi linaloikumba timu yake katika wakati mgumu wa kuamua hatma ya msimu wao.
Alhamisi hii United inacheza na Celta Vigo ya Hispania kwenye nusu fanaili ya Europa League huku ikiwakosa wachezaji saba wa kikosi cha kwanza.
Mourinho ni kama vile haamini uwajibikaji wa baadhi wa wachezaji wake majeruhi na mara kadhaa amekuwa akitoa kauli zinazoonyesha kuwa ndani ya kuumia kwao, pia kuna ‘madeko’.
Kocha huyo amepiga kijembe na kusema: “Sasa tupo kwenye wakati ambao mtu anaweza hata kutoka kitandani kwenda bafuni na akavunjika mguu”.
United inakabiliwa na msongamano mgumu wa mechi za Europa League na Premier League na ili apate nafasi ya kucheza Champions League msimu ujao, inatakiwa itwae Europa League au imalize nafasi ya nne katika Premier League.
Celta Vigo (A), Europa League, May 4
Arsenal (A), League, May 7
Celta Vigo (H), Europa League, May 11
Tottenham (A), League, May 14
Southampton (A), League, May 17
Crystal Palace (H), League, May 21
Europa League Final (?), May 24

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *