Habari

MOURINHO AWAKATIA TAMAA CHRIS SMALLING NA PHIL JONES

on

Mabeki wa Manchester United Chris Smalling na Phil Jones hawategemewi kuwa fiti kwenye mchezo wa Europa League dhidi ya  Celta Vigo siku ya Alhamisi, hiyo ni kwa mujibu wa Jose Mourinho.
Wachezaji hao wawili wamekuwa nje ya dimba kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya kuumia wakati walipokuwa na timu ya taifa ya England kwenye mechi za kirafiki.
Alipoulizwa kama mabeki hao wa kati watakuwa tayari kwa safari ya Hispania, kocha Mourinho alisema: “Sidhani kama wataweza. Hii ni kwa mtazamo wangu binafsi.
“Sijui kama tutakuwa nao lakini najua wachezaji nitakaowachagua watafanya vizuri. Kwahiyo haijalishi kama tutakuwa na na Darmian kama sentahafu, kama ni Carrick au Axel, nawaamini vijana wangu.
“Ari ipo juu, Marouane Fellaini na Paul Pogba watarejea uwanjani kwahiyo angalau tuna chaguo la kutosha.”
Janga la majeruhi limeendelea kuiandama Manchester United baada ya mabeki Luke Shaw na Eric Bailly kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Swansea Jumapili mchana.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *