MPANGO WA MKWASA WA MASHABIKI KUICHANGIA YANGA WAANZA KUZAA MATUNDA

BAADA ya katibu mkuu wa Yanga Charles Bonifasi Mkwasa kutangaza juu ya mpango maalum kwa wanachama wake kuichangia, klabu hiyo umeanza kuzaa matunda ambapo wadau mbalimbali wameanza kujitokeza.

Yanga ambayo tangu iwe chini ya mwenyekiti wake Yusuph Manji haijawahi kukumbwa na ukata, imekuwa kwenye kipindi kigumu cha mpito tangu mwekezaji huyo alipopatwa na matatizo binafsi hali iliyosababisha akose muda wa kuihudumia timu.

“Tuna malengo ya kupata walau milioni nne kwa siku na hili linaweza kusaidia kupunguza mzigo wa gharama za kuendesha timu,” alisema Mkwasa.

Mpaka kufika jioni ya mwishoni mwa wiki iliyopita, tayari Yanga ilikuwa imeingiza kiasi cha sh. mil 9.5 toka kwa wanachama wake ambao walijitokeza kuchangia.

Yanga iriripotiwa kuwa na harufu ya mgomo ambayo ilitokana na baadhi yawacheaziji kutolipwa mishahara yao kwa wakati huku ikiwa katikati ya ratiba ngumu ya michezo ya kimataifa dhidi ya MC Alger ya nchini Algeria.

No comments