MPIGA SOLO WA TOT BAND AFARIKI DUNIA …ni Mirage Halitopo


Mpiga solo wa TOT Band, Mirage Halitopo (pichani juu) amefariki dunia mchana huu.

Mirage aliyeletwa hapa nchini na Ally Chocky mwishoni mwa miaka ya 2000, amefia katika hospitali ya Mwananyamala alikokuwa amelazwa tangu juzi juzi.

Mpiga solo huyo alikuwa akiugulia nyumbani kwa takriban mwezi mzima kabla ya kulazwa Mwananyamala Hospital.
Habari zaidi zitafuata baadae.

Huyu anakuwa msanii wa pili wa TOT kufariki ndani ya miezi miwili. Wa kwanza alikuwa ni mpiga bass Samwel Mshana aliyefariki Aprili 8 ambaye alikuwa swahiba mkubwa wa Mirage.


No comments