MSAFIRI DIOUF ASHINDWA KUREKODI NYIMBO UINGEREZA


Rapa na mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta Msafiri Diouf ambaye kwasasa anafanya kazi huko England, ameshindwa kurekodi wimbo wake wowote Ulaya kutokana na gharama za studio kuwa juu.

Akiongea na Saluti5, Diouf amesema ana nyimbo zisizopungua nne, lakini ameshindwa kurekodi hata mmoja na hivyo jambo hilo litasubiri hadi siku atakaporejea Tanzania.

“Kwasasa huwezi kupata nyimbo yangu mpya, studio huku mpaka nyimbo ikamilike sio chini ya pauni 1200 (zaidi ya sh. 3,300,000 za Kitanzania). Kwahiyo nimeona bora nije kurekodi Bongo,” amesema Diouf.

Msanii huyo aliyetamba pia na Twanga Chipolopolo, amesema anatarajia kuja Tanzania baadae mwaka huu ambapo ameahidi kurekodi nyimbo zinazoendana na soko la sasa.

No comments