MSAFIRI DIOUF: NAKUJA KIVINGINE SITAJALI NIKIAMBIWA DANSI LIMENISHINDA


Msafiri Diouf, nyota wa zamani wa Twanga Pepeta na Twanga Chipopolo ambaye anafanya kazi za muziki nchini England, amesema anakuja na mabadiliko makubwa kwenye muziki wake.

Mwanamuziki huyo anasema sio kwamba muziki wa dansi wa sasa sio mzuri ila ukweli ni kwamba kila kizazi na muziki wake.

Anasema hata Awilo Longomba alichungulia soko na kujiongeza na sasa anapiga ‘kolabo’ na Wanigieria, anapiga pesa kama kawaida.

Diouf amesema atapiga nyimbo ambazo zinaweza kuchezwa Burundi, Rwanda, Kenya, Tanzania na kwingineko.
Msafiri Diouf anasema kizazi (generation) hiki ni tofauti sana na cha zamani, cha msingi ni kujiuliza mashabiki wa sasa wanapenda nini katika muziki halafu unaenda nao sawa.

“Wazungu wasema kama huwezi kuwapiga, basi ungana nao. Nitapiga muziki unaohitajika sokoni, sitajali watakaosema dansi limenishinda,” alisema Diouf katika mazungumzo yake na Saluti5.

“Tena kabla sijarekodi nitamfatuta msanii wa bongo fleva anipe ushauri zaidi namna ya kuendana na kasi ya soko kisha nitachanganya na uzoefu wangu. Nitapiga muziki wa biashara,” aliongeza Diouf.

Nyimbo anazotarajia kuibuka nazo Diouf ni “ The Bridges”, “Waka Waka”, “Show Me Your Love 4 D.R.E – Repulic of East Africa” na “Come Together”.

No comments