MSONDO NA SIKINDE KUPAMBANA MEI 20 TRAVERTINE …wasema kunyonywa sasa basi


Bendi kongwe zenye upinzani wa jadi hapa nchini Msondo Ngoma (Tucta Jazz Band) na Sikinde Ngoma ya Ukae (Mlimani Park Orchestra), zatampana Jumamosi ya Mei 20.

Onyesho hilo la ‘Nani Zadi’ litafanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni.

Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, mratibu wa onyesho hilo Abdulfareed Hussein ambaye ni seneta wa Msondo, alisema bendi hizo sasa zimeamua kuandaa wenyewe.

Naye Mjusi Shemboza wa Sikinde akasema kuwa mara nyingi maonyesho yao ya ‘Nani Zaidi’ walikuwa wakiyakabidhi kwa mapromota ambao walitengeneza faida kubwa huku bendi zikiambulia pesa kiduchu.

“Sasa inatosha, kunyonywa basi. Kuanzia sasa tutakuwa tunaratibu wenyewe maonyesho yetu ya pamoja,” alisema Shemboza.

Abdulfareed ametamba kuwa onyesho hilo litakuwa lililokwenda shule, jukwaa la kisasa, sound ya kisasa na mapambo ya kisasa.

“Tutafunga jukwaa siku mbili kabla na tutalifanyia majaribio ya awali (rehearsal)” alisema Abdulfareed.
Baadhi ya wawakilishi wa Msondo kwenye mkutano wa waandishi wa habari
Baadhi ya wawakilishi wa Sikinde kwenye mkutano wa waandishi wa habari
No comments